Mwamba Aliyefariki na Kuzikwa Aonekana Akikatiza Mitaa ya Arusha

Mtu mmoja anayefahamika kwa jina la Robert Lukumay Mkazi wa kijiji cha Olgililai katika kata Ya kiutu Wilayani Arumeru Mkoani Arusha anadaiwa kuonekana baada ya kufariki na kuzikwa May 31,2024 nakuzikwa


Baba mdogo wa marehemu amesema ni kweli waliuzika mwili wake lakini ameshangaa kumuona tena huku akidai kwamba awali kulikuwa na mgogoro wa Robert akitaka kuuza shamba la alilopewa lakini familia ilimkatalia nakuongeza kuwa endapo atashinikiza tena kuhusu shamba hilo hawataruhusu aliuze hata kama amefufuka


Robert Lukumay anayedaiwa kufa na kufufuka akizungumza amedai kuwa amekuwa akiishi Ngarenaro na alionekana na ndugu yake nakumuita huku akikanusha taarifa hizo za kuzikwa nakusema alikuwa anaishi kwa rafiki yake


Hadi hivi sasa haijabainika ni mwili wa nani uliozikwa May 35,2024 licha ya Mchungaji aliyeendesha ibada ya mazishi akidai kuwa aliyeonekana ndiye aliyezikwa

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii