Kiambu - Aliyekuwa Jaji Mkuu Willy Mutunga ameungana na wanaharakati kutetea haki za waandamanaji waliotekwa nyara.
Rais huyo wa zamani wa Idara ya Mahakama alionyesha hasira yake kutokana na kuongezeka kwa kamatakamata, mashambulizi na utekaji nyara, akibainisha kuwa vinakiuka masharti ya katiba.
Mutunga alikuwepo katika makao makuu ya DCI kaunti ya Kiambu, ambapo waandamanaji walianza kuimba nyimbo za maandamano kuheshimu wahamasishaji wa kupinga mswada wa fedha. "Utekaji nyara ni kinyume cha sheria. Polisi wanastahili kuzingatia katiba na vipengee vya haki za binadamu," alisema kwenye video iliyosambazwa na NTV Kenya.