Mahakama yapinga Gachagua kung'olewa

Mahakama Kuu nchini Kenya imesitisha kwa muda utekelezwaji wa azimio la Bunge la Seneti juu ya hoja ya kumuondoa madarakani Naibu Rais wa Kenya Rigathi Gachagua.


Uamuzi huo wa Mahakama umetolewa leo Oktoba 18, 2024 na Jaji Chacha Mwita ambapo mbali na kuzuia kutekelezwa kwa azimio hilo pia Mahakama imezuia Rais William Ruto kuteua mtu mwingine kuchukua nafasi hiyo hadi Oktoba 24, 2024 kesi hiyo itakaposikilizwa na Jopo la Majaji watakaoteuliwa na Jaji Mkuu Martha Koome.

Hayo yote yanajiri wakati ambao tayari Rais wa Kenya, William Ruto akiwa amemteua Waziri wa Mambo ya Ndani Profesa Kithure Kindiki kuichukua nafasi ya Rigathi Gachagua na Bunge la Taifa limeafiki uteuzi wake.

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii