Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP Simon
Sirro amesema kamwe Jeshi hilo alitavumilia vitendo vya kujichukulia
sheria mkononi vinayofanywa na baadhi ya watu wa jamii ya wakulima na
kifugaji ambapo katika wilaya ya Kilindi mkoani Tanga zaidi ya watu 20
wanashikiliwa na Jeshi la Polisi kutokana na mapigano ya wakulima na
wafugaji yaliyotokea Januari 30 katika kata ya Kibirashi na Elerai na
kusababisha vifo vya watu sita.
IGP Sirro ametoa kauli hiyo
wakati alipofanya ziara ya kutembelea wilaya ya Kilindi mkoani Tanga kwa
lengo la kuzungumza na wananchi mbalimbali wa jamii za kifugaji na
wakulima ambao wameathirika kutokana na mapigano yaliyohusisha jamii
hizo mbili na kusababisha vifo pamoja na majeruhi.