Watu waandamana mbele ya Bunge la Kenya kupinga ushuru mpya

Watu kadhaa wamekusanyika mbele ya Bunge la Kenya leo Jumanne kupinga rasimu ya bajeti ya mwaka 2024-2025 ambayo inatoa kodi mpya, huku polisi wakitumia gesi ya kutoa machozi na kukamata angalau watu watatu.

Sehemu ya kwanza ya matumizi iliidhinishwa na Bunge, ambapo Rais William Ruto ana wingi wa wabunge, lakini ile ya mapato - haswa kutoa ushuru wa kila mwaka wa 2.5% kwa magari ya kibinafsi na kurejeshwa kwa VAT kwenye mkate - imepataukosoaji mkubwa. Wabunge wataanza kuchunguza rasimu hii leo Jumanne alasiri, rasimu ambayo itapigiwa kura kufikia tarehe 30 Juni.


Takriban watu watatu wamekamatwa wakati wa maandamano hayo, amebainisha mwandishi wa habari wa shirika la habari la AFP. Polisi, waliotumwa kwa wingi mbele ya makao makuu ya Bunge na katikati mwa jiji la mji mkuu, pia walitumia gesi ya kutoa machozi. Vuguvugu la maandamano linaloitwa "Occupy Parliament" lilianza kwenye mitandao ya kijamii baada ya mwanaharakati kuvujisha namba za sim za wabunge mtandaoni ili waweze kupigiwa simu kuwahimiza kutoipigia kura rasimu ya bajeti.


Sera ya ushuru ya Mkuu wa Nchi, tangu kuchaguliwa kwake Agosti 2022, imekuwa chanzo cha hasira. Bw. Ruto, ambaye alikua msemaji wa watu wanyonge zaidi wakati wa kampeni za uchaguzi, haswa aliongeza ushuru wa mapato na michango ya afya na kuongeza mara mbili ya VAT kwenye petroli, hadi 16%. Hatua hizi, zilizotetewa na serikali ili kuziba pengo katika nchi hii yenye karibu wakaazi milioni 51, zilisababisha maandamano ya upinzani mwaka jana, ambayo wakati mwingine yalisababishwa na ghasia mbaya.


Mojawapo ya nchi zilizoendelea kiuchumi katika Afrika Mashariki, Kenya ilirekodi mfumuko wa bei wa 5.1% kwa mwaka mwezi wa Mei, huku bei ya chakula na mafuta ikipanda kwa 6.2% na 7% mtawalia, kulingana na data ya Benki Kuu. Ukuaji wa Pato la Taifa unatarajiwa kushuka hadi 5% mwaka huu, baada ya kufikia 5.6% mwaka 2023 (4.9% mwaka 2022), kulingana na utabiri wa Benki ya Dunia. Deni la umma la nchi linafikia karibu shilingi bilioni 10,000 (EUR bilioni 71), au karibu 70% ya Pato la Taifa.

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii