Pacha walioungana mmoja aingia kwenye ndoa

Abigail Loraine Hensel na Brittany Lee Hensel, ni moja kati ya pacha waliopata umaarufu kupitia Tamthilia ya ''Abby & Brittany'' inayorushwa kupitia TLC.


Abigail Loraine Hensel anachukua nafasi muda huu kwenye mitandao ya kijamii na hii ni baada ya kuingia kwenye ndoa na mwanajeshi mstaafu kutokea Jeshi la Marekani anayefahamika kama Josh Bowling


Abby na dada yake pacha Brittany, Ni pacha walioungana kiwiliwili na viungo vya chini ilikuwa ni ngumu kwa wao kutengenishwa wakiwa wadogo na hii ni kutoka na uwezekano mdogo wa kuishi baada ya kutengenisha na badala yake wazazi kuamini kuwa wanaweza kufikia kwenye malengo yao wakiwa kwenye hali ambayo wako nayo.


Kwa sasa Abby na dada yake pacha Brittany, Ni waalimu wa shule ya msingi kwenye jimbo wanalotokea la Minnesota nchini Marekani.

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii