Ajali ya kushangaza yajeruhi, yaleta uharibifu

Ajali ya magari mawili kugongana imesababisha majeruhi na uharibifu eneo la kashura lililopo Manispaa ya Bukoba Mkoani Kagera.

Akizungumza na vyombo vya habari katika eneo la tukio Mkuu wa Wilaya Bukoba, Erasto Sima amesema ajali hiyo imehusisha gari la Costa lenye namba T117 EBD kugongana na Landcruiser yenye namba T678 DHM Maeneo ya Mlima wa Kashura Kata Bakoba Manispaa ya bukoba Mkoani Kagera.

Amesema kwenye ajali hiyo saa 4 na nusu asubuhi kwenye Costa walikuwemo abilia watano na kwenye landcruiser walikuwemo abilia wawili na mpaka na hakuna vifo ambapo majeruhi wote walikimbizwa katika Hospitali ya rufaa Bukoba.

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii