Daktari wa Biden asema yuko imara kutekeleza majukumu yake

Daktari wa Rais wa Marekani Joe Biden amesema kuwa kiongozi huyo yuko katika hali nzuri kuongoza na hakuna wasiwasi wowote wa kiafya.


Hii ni baada ya rais huyo mwenye umri wa miaka 81 kufanyiwa uchunguzi wa mwisho wa matibabu kabla ya uchaguzi Biden na Trump washinda michujo yao Michigan huku umri wake ukionekana kuwa suala muhimu.

Ripoti hiyo ya uchunguzi wa kila mwaka iliyosubiriwa kwa hamu katika hospitali ya kijeshi ya Walter Reed nje ya mji wa Washington imetolewa wiki chache tu baada ya ripoti ya mwanasheria maalum kumuonyesha kuwa ni mzee na msahaulifu.

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii