“Kuna uwezekano mkubwa ikiwa mapigano yataendelea na kuna hatari yataibuka katika maeneo yenye msongamano mkubwa wa watu kusini mwa Gaza. Kwa hivyo tunasisitiza wito wetu wa kusitisha mapigano, “ alisema Ramesh Rajasingham, mkurugenzi wa Ofisi ya Umoja wa mataifa ya kuratibu misaada ya kibinadamu.
Mtoto mmoja kati ya watoto sita walio na umri wa chini ya miaka miwili kaskazini mwa Gaza anakabiliwa na utapiamlo mkali na kupoteza uzito wa mwili, na takriban watu wote milioni 2.3 katika eneo la Palestina wanategemea chakula kisichotosha ili kuishi, aliliambia Baraza la usalama la Umoja wa mataifa.