MLIMBWENDE AFARIKI BAADA YA KUJIRUSHA KUTOKA GHOROFANI

Aliyewahi kushika taji la Miss USA Cheslie Kryst amefariki siku ya Jumapili akiwa na umri wa miaka 30 baada ya kuruka kutoka katika jengo refu huko Manhattan, New york.

Polisi pamoja na familia yake wamethibisha kifo cha mlimbwende huyo aliyetawazwa kuwa Miss USA mwaka 2019.
Kulingana na polisi, mwili wa Kryst ulipatikana majira ya saa moja asubuhi mbele ya jengo refu la Orion.

Mlimbwende huyo alikuwa akiishi kwenye jengo hilo gorofa ya tisa lakini mara ya mwisho alionekana juu ya ghorofa ya 29.

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii