Ibaada ya mazishi ya mwanariadha Kelvin Kiptum inaendelea

Mshikilizi wa rekodi ya dunia katika mbio za masafa marefu upande wa wanaume, Kelvin Kiptum, anatarajiwa kuzikwa hii leo Ijumaa nyumbani kwake katika kaunti ya Elgeyo-Marakwet mkoa wa bonde la ufa nchini Kenya.


Rais wa Kenya William Ruto anawaongoza waombolezaji katika kumuenzi mwanariadha huyo aliyevunja rekodi ya dunia akiwa na umri mdogo.  

Kiptum alifariki katika ajali ya gari, akiwa na umri wa miaka 24 wiki mbili zilizopita pamoja na kocha wake raia wa Rwanda Gervais Hakizimana.



Maelfu ya raia hapo jana walitoa  heshima kwa Kiptum katika mji wake wa asili.

Umati wa watu ulikusanyika njiani mjini Eldoret wakati mwili wake ukipelekwa nyumbani kwao kwa ajili ya ibaada ya mazishi.

Alikuwa amejiwekea malengo ya kukimbia mbio ndogo za saa mbili za marathon huko Rotterdam mwezi huu wa Aprili. Kiptum alikuwa mtoto peke katika familia yao.

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii