Mjumbe wa Kamati kuu ya CCM, Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Tabora Ndugu Hassan Wakasuvi amefariki Dunia.
Chama Cha Mapiduzi kikiongozwa na Mwenyekiti wake na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan , kimepokea kwa masikitiko makubwa na kutoa salamu za rambirambi na pole kwa ndugu, jamaa, marafiki na wanachama wote kufuatia kifo cha Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Tabora Hayati. Hassan Wakasuvi.