Wakati huu dunia, ikiadhimisha siku ya kimataifa ya wanawake, wanawake katika nchi zinazoendelea wanalazimika kubeba mzigo mkubwa wa kuwa walezi wa watu kwenye jamii hasa wanaougua magonjwa yasiyoambukizwa ambayo husababisha vifo vya watu milioni 41 duniani kwa mujibu wa shirika la afya, WHO.
Kufikia mwaka 2030,asilimia 74 ya vifo duniani vitakuwa vinasababishwa na magonjwa yasiyoambukiza ,asilimia zaidi ya sabini vikichangiwa na mataifa yanayoendelea.
Idadi hii kubwa ya wagonjwa wanaougua magonjwa haya,linawalazimu wanawake wengi kuwa walezi.
Jenniffer Birir kutoka kaunti ya Bomet amekuwa akihudumia mgonjwa wa kisukari.
"Ukiwa na mgonjwa, hakuna mahali pakwenda, unamhudumia tu kila wakati." alieleza Jenniffer Birir.