Umoja wa Mataifa unakadiria kuwa mapaka kufikia mwishoni mwa mwaka 2023, watu milioni saba walikimbia makazi yao nchini DRC, wakiwemo milioni 2 na laki 5 katika jimbo la Kivu Kaskazini pekee.
hirika la kimataifa la kutetea haki za Binadamu, Human Rights Watch, limechapisha ramani yake inayoashiria maendeleo ya hali ya Haki za binadamu likitoa wito kwa Rais wa DRC, Félix Tshisekedi kuzingatia zaidi masuala ya haki za binadamu katika kipindi hiki cha muhula wake wa pili.
Katika Nyaraka zilizochapishwa hivi karibuni, Human Rights Watch imeitaka serikali ya Congo kuzingatia uhuru wa watu kujieleza na usalama wa raia katika maeneo yenye migogoro.
Thomas Fessy ni mtafiti mkuu wa shirika hilo nchini DRC.
“Kwa bahati mbaya sana ahadi nyingi zinaonekana kutotekelezwa ukizingatia kukamatwa kwa watu kiholela na vitisho kadhaa dhidi ya wanaharakati.” alisema Thomas Fessy ni mtafiti mkuu wa HRW nchini DRC.