Vikundi 345 Vimekidhi Vigezo Vya Kupewa Zabuni


NAIBU Waziri Ofisi ya Rais-TAMISEMI anayeshughulikia Afya, Dkt Festo Dugange amesema Serikali za Mitaa zimeweka utaratibu wa kusajili makundi maalum ya wanawake, vijana na wenye ulemavu ambapo ameeleza zaidi ya vikundi maalum 345 vimesajiliwa katika halmashauri ambavyo vimekidhi vigezo vya kupewa zabuni.

Mhe Dkt Dugange ametoa kauli hiyo leo wakati akijibu maswali ya wabunge katika kikao cha kwanza cha mkutano wa 14 wa Bunge la 12 ulioanza leo jijini Dodoma.

Akijibu swali la Mbunge wa Viti Maalum, Shally Raymond aliyeuliza ni Zabuni ngapi zilizotolewa na Halmashauri za Majiji, Manispaa na Wilaya kwa makundi maalum hasa Wanawake kama sheria inavyotaka, Mhe Naibu Waziri Dkt Dugange amesema,

“ Kwa mujibu wa sheria ya ununuzi wa umma ya mwaka 2011 ma marekebisho yake ya mwaka 2016 katika kifungu cha 64 (2) (c) na tangazo la Serikali Na. 333 la mwaka 2016, taasisi zinapaswa kutenga asilimia 30 ya manunuzi kwa ajili ya makundi maalum.

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii