Korea Kaskazini yarusha makombora kadhaa baharini

Jeshi la Korea Kusini limesema kuwa Korea Kaskazini ilirusha makombora kadhaa katika Pwani yake ya Mashariki.

Hii ikiwa ni mara ya pili kwa Pyongyang kufanya majaribio ya aina hiyo ya silaha katika kipindi chini ya wiki moja.

Kulingana na taarifa hiyo makombora hayo yalirushwa majira ya saa mbili asubuhi na kwamba mamlaka za kiitelijensia za Marekani na Korea Kusini zinafanya tathmini.

Hata hivyo haikuelezwa ni makombora mangapi yaliyorushwa na kiasi cha umbali yaliyosafiri.


Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii