Takriban magaidi 60 wameuwawa nchini Burkina Faso na vikosi vya ndani vikisaidiwa na vile vya Ufaransa vilivyo pelekwa nchini humo kwa mujibu wa taarifa ya jeshi la Ufaransa.
Taarifa ya jeshi la Ufaransa imeeleza kwamba mara nne kati ya Januari 16 na Januari23, mwaka huu, makundi ya magaidi yalitasakwa na kushambuliwa na vikosi vya Burkina Faso ambapo magaidi 60 waliuwawa.
Burkina Faso imekuwa ikikabiliwa na mashambulizi ya wanamgambo wenye msimamo mkali toka mwaka 2015, wakati wanamgambo wenye uhusiano na Al-Qaida, na Islamic State walipoanza kuvuka mpaka na kufanya mashambulizi kutokea Mali.
Zaidi ya watu 2,000 wamefariki dunia kwa mujibu taarifa zilizokusanywa na shirika la habari la AFP. Idara ya dharura ya kitaifa inaeleza kwamba watu milioni 1.5, takribani theluthi tatu ni watoto awali walikoseshwa makazi tokea Novemba 30, 2021