Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky ametoa wito wa uchunguzi wa kimataifa kuhusu ajali ya ndege ya jeshi la Urusi iliyotokea Jumatano katika eneo la mpaka wa Belgorod Magharibi mwa Urusi.
Katika hotuba yake ya jana jioni, Zelensky amesema kuwa huduma ya ujasusi ya kijeshi ya Ukraine HUR, kwasasa, inajaribu kuchunguza zaidi kuhusu hatima ya wafungwa wa kivita wa nchi hiyo ambao kulingana na Urusi walikuwa ndani ya ndege hiyo.
Zelensky pia amemuagiza waziri wa mambo ya nje wa nchi hiyo Dmytro Kuleba kutoa habari zote zinazojulikana na Ukraine kwa washirika wa kimataifa.
Kulingana na ripoti zaUrusi, ndege hiyo ya kijeshi aina ya Ilyushin chapa II-76 ilikuwa na abiria 74 ambao wote wamefariki.
Hata hivyo, hakuna habari huru kuhusu nani ama nini kilichobebwa ndani ya ndege hiyo.