Wanaharakati Marekani waendeleza kampeni kupinga vita Gaza

Wanaharakati wamewahimiza wapiga kura kuandika maneno "sitisha mapigano" wakati wa kura za mchujo za kuteua mgombea wa urais kama sehemu ya kupinga jinsi Rais Joe Biden anavyoshughulikia mzozo kati ya Israel na Hamas.

Muungano wa wanaharakati wa kupinga vita vinavyoendelea ukanda wa Gaza, umesema hatua hiyo itawapa nafasi Wamarekani kupaza sauti zao dhidi ya Rais Biden kutokana na vifo vya raia huko Gaza.

Wapiga kura katika jimbo la Kaskazini Mashariki la New Hampshire watashiriki kura za mchujo leo na wito huo wa kuandika maneno "sitisha mapigano" kwenye karatasi za kura unalenga kuushinikiza utawala wa Biden.

Wanaharakati hao wameandika kwenye mtandao wa kijamii wa X, kuwa utawala wa Biden kwa muda wa miezi mitatu iliyopita, umepuuza miito ya kutaka kusitishwa kwa vita na kukomesha uungwaji mkono wao kwa Israel.


Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii