Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron anaonekana kwenye runinga Jumanne hii, Januari 16, kuelezea mkondo wake, siku chache baada ya kuteuliwa kwa serikali iliyo na wajumbe wengi kutoka mrengo wa kulia na ambayo tayari inakabiliwa na mizozo ya kwanza. Fuata hotuba ya Emmanuel Macron.
Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron anaanza hotuba yake ya utangulizi kwa kutetea matokeo ya sehemu ya kwanza ya muhula wake wa pili wa miaka mitano: “Tumeunda zaidi ya nafasi za kazi milioni 2, zaidi ya viwanda 300 […]. Tumewekeza tena kwa kiasi kikubwa katika majeshi yetu, kwa maafisa wetu wa polisi, vyeo vyetu, kwa mfumo wetu wa mahakama, lakini pia kwa shule zetu na afya zetu [...]. Tuna silaha bora kuliko miaka sita na nusu iliyopita. "
Emmanuel Macron anakiri, hata hivyo, kwamba "hakuwa amebadilisha (mambo) kwa kiasi kikubwa" dhidi ya "uamuzi wa kijamii na familia". "Mustakabali wa watoto wa Jamhuri bado unabaki kuamuliwa sana na jina la familia, mahali ambapo mtu alizaliwa, mazingira ambayo mtu huyo anaishi. Ni dhuluma mbaya zaidi, ukosefu wa usawa tangu mwanzo” wakati "ahadi ya Republican ni ile ya usawa wa fursa".
Emmanuel Macron amesema ameshawisika Jumanne jioni kwamba "watoto wetu wataishi vizuri zaidi kesho": "Nataka hapa kujaribu kuelezea maana ya kina ya kitendo hiki, kimsingi kuifanya Ufaransa kuwa na nguvu zaidi na ya haki," amesema rais wa Jamhuri wakati wa mkutano na waandishi wa habari. "Nina hakika kwamba tuna kila kitu cha kufanikiwa" na kwamba "hatujamaliza historia yetu ya maendeleo na kwamba watoto wetu wataishi bora kesho kuliko tunavyoishi leo". Na hii, rais anathibitisha, ni kutokana na serikali ambayo "iliyo na nguvu na changa zaidi" ya Jamhuri ya Tano.