Kigali yakosoa kauli ya Marekani kuhusu ongezeko la machafuko mashariki ya DRC

Aidha Kigali imeeleza kuwa jumuiya ya kimataifa haijali kutokana na kile imedai kuwa ni shughuli za kijeshi zinazoendelezwa na DR Congo na kwamba operesheni kubwa za nchi hiyo huko Kivu Kaskazini ni kinyume na maamuzi ya taratibu za kikanda.

Wanajeshi kutoka Jumuiya ya SADC wamekuwa wakiwasaidia wanajeshi wa DRC katika vita vyake dhidi ya makundi yenye silaha ikiwemo M23.

Kigali yakosoa kauli ya Marekani kuhusu ongezeko la machafuko mashariki ya DRC

Nairobi – Nchi ya Rwanda imeituhumu Marekani kwa kuikosoa kutokana na ongezeko la machafuko mashariki mwa nchi ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo wakati pia ikieleza kuguswa na kile imesema ni kupuuzwa kwa mchakato wa upatikanaji wa amani kwenye ukanda.

[Image d'illustration] Des personnes se rassemblant à côté de véhicules de la Force de défense nationale sud-africaine (SANDF) dans le cadre de la mission de la Communauté de développement de l'Afriqu
Wanajeshi kutoka Jumuiya ya SADC wamekuwa wakiwasaidia wanajeshi wa DRC katika vita vyake dhidi ya makundi yenye silaha ikiwemo M23. AFP - AUBIN MUKONI
MATANGAZO YA KIBIASHARA

Aidha Kigali imeeleza kuwa jumuiya ya kimataifa haijali kutokana na kile imedai kuwa ni shughuli za kijeshi zinazoendelezwa na DR Congo na kwamba operesheni kubwa za nchi hiyo huko Kivu Kaskazini ni kinyume na maamuzi ya taratibu za kikanda.

Wanajeshi kutoka Jumuiya ya SADC wamekuwa wakiwasaidia wanajeshi wa DRC katika vita vyake dhidi ya makundi yenye silaha ikiwemo M23.

Wanajeshi wa SADC wanawasaidia wenzao wa DRC kupamabana na makundi ya watu wenye silaha.
Wanajeshi wa SADC wanawasaidia wenzao wa DRC kupamabana na makundi ya watu wenye silaha. AFP - AUBIN MUKONI

Wiki iliopita, maofisa wawili wa jeshi la Afrika Kusini ambao ni sehemu ya walinda amani wa SADC waliuawa wakati wengine watatu wakijeruhiwa katika mlipuko kwenye kambi yao.

Wikendi iliopita, Marekani iliituhumu Rwanda inayodaiwa kuwaunga mkono waasi wa M23 nchini DR Congo na kuwataka waasi hao kuondoka mara moja kwenye ardhi ya Congo.

Kigali kwa upande wake imeendelea kukanusha madai kwamba inawaunga mkono na kuwafadhili waasi wa M23 ambao wanayumbisha usalama wa mashariki mwa RDC.

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii