Urusi kutozivamia Poland, Latvia

Rais Vladimir Putin wa Urusi amesema hana mpango wa kuivamia Poland, Latvia ama eneo jingine lolote na wala hana nia ya kuvipanua vita vyake nchini Ukraine.

Putin amesema hayo kwenye mahojiano na mtangazaji wa televisheni wa nchini Marekani Tucker Carlson yaliiyorekodiwa siku ya Jumanne mjini Moscow.

Lakini Putin amesisitiza kwamba watachukua hatua ikiwa Poland itaivamia Urusi na kuongeza kuwa hana maslahi yoyote nchini humo wala Latvia na eneo jingine lolote na kwa maana hiyo hawaoni sababu ya kuwavamia.

Putin aidha ameyahakikishia mataifa ya Magharibi kwamba kamwe Urusi haitashindwa katika vita vyake nchini Ukraine na kuitaka Jumuiya ya Kujihami ya NATO kukubaliana na hatua ya Urusi ya kuyanyakua maeneo nchini humo.

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii