Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kilimanjaro, Simon Maigwa amethibitisha kukamatwa kwa watu hao, ambapo amesema miongoni mwao yupo kinara ambaye ni kiongozi wa mtandao wa ‘vishoka’ mkoani humo.
“Tumeshakamata kiongozi wao mkubwa wa hicho kikosi ambaye amekuwa akishirikiana na mtandao mkubwa ambao upo ndani ya watumishi hawa wa Tanesco, wote hawa tumewakamata na tuko kwenye hatua nzuri,”alisema Kamanda Maigwa
Mkuu wa Wilaya ya Moshi, Kisare Makori alisema watu hao wamekuwa wakiihujumu serikali kwa manufaa yao wenyewe na kuikosesha serikali mapato yake.