Uturuki yadaiwa kufanya mashambulizi ya anga ndani ya Syria

Vyanzo vya ndani pamoja na chombo cha habari cha serikali ya Syria wamesema Jumatatu kwamba Uturuki imefanya mashambulizi kadhaa ya anga kwenye miundombinu ya umeme na mafuta kwenye eneo la kaskazini mashariki mwa Syria, linalishikiliwa na wa Kurdi, na kupelekea huduma za umeme kukatika.

Hogir Najar ambaye ni afisa wa habari kwenye utawala wa Kikurdi ameambia Reuters kwamba takriban maeneo 40 yamelengwa kwa mabomu ya Uturuki ndani ya siku mbili zilizopita, ikiwemo kwenye vituo vya kuzalisha umeme, mamboma ya maji pamoja na mifumo ya mafuta. Najar ameongeza kusema kwamba takriban miji 10 iliyopo karibu na mpaka haina huduma za umeme wala maji kutokana na mashambulizi hayo.

Uturuki kwa muda saa imekuwa ikifanya mashambulizi ya mabomu dhidi ya kundi la kijeshi la wa Kurdi la YPG ndani ya Syria, ikiamini kuwa ni sehemu ya lile lililopigwa marufuku ndani ya Uturuki la Kurdistan Workers Party, au PKK. Kundi hilo tayari limeorodheshwa kuwa la kigaidi na Uturuki, Marekani, na EU, na limekuwa likipigana na serikali ya Uturuki tangu 1984.

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii