P Diddy Atuhumiwa Kwa Ubakaji Katika Kesi Mpya

Mtayarishaji Muziki na Mfanyabiashara, Sean Combs Diddy amefunguliwa mashtaka na Joi Dickerson-Neal ambaye amemtuhumu kumpa Dawa za Kulevya kisha kumdhalilisha Kingono, tukio lililotokea Januari 3, 1991.

Mlalamikaji anadai baada ya kupewa Dawa na kudhalilishwa aligundua Diddy au PuffDaddy au P. Diddy alirekodi tukio hilo kwa siri na kuwaonesha watu kadhaa.

Mwanasheria wa Diddy amedai tuhuma hizo ni za kutunga na mhusika ana nia ya kujipatia Fedha

Hivi karibuni Diddy pia alikabiliwa na tuhuma za aina hiyo kutoka kwa aliyekuwa mpenzi wake, nyota wa R&B, Casandra Ventura (Cassie) lakini walimaliza shauri lao nje ya Mahakama.

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii