Maafisa wa Israel na wapiganaji wa Hamas, walitangaza Jumanne kwamba wamekubaliana juu ya usitishaji mapigano wa siku nne ili kuwezesha kundi la wanamgambo kuwaachia huru mateka 50 kati ya karibu 200 wanaoshikiliwa.
Baraza la mawaziri la waziri mkuu Benjamin Netanyahu lilidhinisha makubaliano hayo baada ya majadiliano ya karibu usiku mzima ambapo mawaziri walokua wanapinga makubaliano hayo walisema huu ulikua ni uwamuzi mgumu lakini ni uwamuzi ulo sahihi.
Viongozi wa Dunia wapongeza Makubaliano
Rais Biden amesema “nimefurahishwa kupita kiasi kwamba baadhi ya watu hawa hodari wataungana tena na familia zao mara tu makaubaliano yatatekelezwa kikamilifu.”
China, Ujerumani, Ufaransa zimekua nchi za kwanza kupongeza makubaliano hayo yaliyofikiwa kutokana na upatanishi wa Qatar.