Rayvanny Athibitisha Kumuoa Fahyma

Staa wa Bongo Fleva, Raymond Mwakyusa 'Rayvanny' amethibitisha kwamba siku sio nyingi atamuoa mpenzi wake wake Fahyma.


Kauli hiyo ya kishujaa ameitoa usiku wa kuamkia leo Agosti 23, 2023 kwenye party bethidei yake ambayo alifanyiwa sapraiz na mpenzi wake huyo.


"Sikutegemea kama kutakuwa na watu wengi, ilikuwa niende kwenye shoo Kongo lakini akanipigia sana simu nije nyumbani lakini nikajua mambo ya ndani tu akanitoa huku nje ndio nakuta kijiji cha watu. "Namshukuru kwa kuniandalia bethidei maana najua ametumia fedha, nawashukuru mliokuja ingawa sikujua kama mpo lakini nimefurahi na nitamuoa soon," alisema Rayvanny.

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii