Wazazi Wamlipisha Binti Yao Kodi ya Nyumba kisa kukataa shule

Wanandoa wa Marekani ambao walianza kumtoza binti yao kodi ya nyumba baada ya kukataa kujiunga na chuo kikuu wamezua mjadala kuhusu malezi ya kisasa.

Uamuzi wao wa kumtoza binti yao mwenye umri wa miaka 19, Kylee Deason, kodi ya Tzs 445,390 kila mwezi ulizua hisia tofauti.

Binti huyo alihitimu shule ya upili mnamo Mei 2022, na Juni 1, ndani ya wiki mbili, alikuwa anawalipa wazazi wake kodi. Uamuzi huo uliwagawa mashabiki wao kuhusu jinsi wazazi wanavyoweza kuwafundisha watoto wao kuwa na utimamu wa kifedha.



Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii