DAVID JAY KUITEKA AFRIKA KIMUZIKI

David Jatta maarufu kwa jina la Sanaa David jay ni Mwimbaji & Mtunzi wa Nyimbo

Mwenye asili ya Denmark na Gambia. Alikulia katika utamaduni ambapo muziki na taswira ilikuwa kubwa  Alizaliwa na kukulia huko Copenhagen.

Kama msanii wa soul/RnB, David Jay alibadilika sana katika miaka michache iliyopita na anakua kwa kasi kama mwimbaji na mtunzi wa nyimbo. Upendo wake na mapenzi yake katika muziki vimemsaidia kutengeneza kiwango bora cha muziki na sauti thabiti ambayo imeweza kuvutia hadhira kubwa sana kimataifa .