Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan ametoa msamaha kwa wafungwa 5,704 katika kuadhimisha miaka 60 ya Uhuru
Akizungumza na wandishi wa habari leo Jumatatu Desemba 27, 2021 Waziri wa Mambo ya Ndani, George Simbachawene amesema Rais Samia ametoa msamaha huo kwa masharti ikiwa ni pamoja na wafungwa hao wawe wametumikia robo ya adhabu zao gerezani na wawe wameingia kabla ya Oktoba 9, 2021.