100 wakamatwa kwa matukio ya kihalifu Temeke

Zaidi ya wahalifu 100 wamekamatwa ndani ya siku mbili wakituhumiwa kujihusisha na vitendo vya uhalifu wa kuvamia nyumba za watu na kupora mali.

Watuhumiwa hao wamekamatwa kufutia uvamizi uliofanywa Septemba 12 na 13 katika kata za Mianzini, Chamazi na Kilungule.

Mkuu wa wilaya ya Temeke, Jokate Mwegelo amesema wahalifu hao wamekamatwa katika msako ulioanza Septemba 14 ambapo doria zinafanyika katika mitaa yote ya wilaya hiyo.

Jokate amesema katika operesheni hiyo hawatawavumilia watendaji wa mitaa wanaotoa ushirikiano kwa wahalifu au kuficha taarifa zao.

“Katika hili niwaambie hatutavumilia, kwahiyo wale wanaokaa vijiweni tutashughulika nao kama wachora ramani za uhalifu. Tutawakamata wote.

“Sitakubali katika uongozi wangu Temeke iingie kwenye dosari ya vitendo vya uhalifu, ndio maana katika hili nasema tutakula sahani moja. Hatuwezi kuwa tunapangiwa kazi na vijana wa hovyo,” amesema Jokate.

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii