"Leo tunashiriki kama wabia kwenye uchimbaji wa rasilimali zetu muhimu na adhimu (mkadini) kwa ajili ya kuliletea maendeleo Taifa letu. Tunapaswa kujipongeza kwa hatua hii.
"Hatua ya safari hii sikuianza mimi, aliianza mwenzetu Dkt John Pombe Magufuli ambaye Mungu alimpa maono na ujasiri akasema hapana, rasilimali zetu sasa imefika wakati zifaidishe wananchi. Niwaombe kila mmoja wetu amuombee kwa Mungu ailaze roho yake mahali pema peponi.
"Moto wa madini aliouwasha Dkt. John Pombe Magufuli nimeupokea, na ninaahidi hautazimika nitakwenda nao." Rais Samia Suluhu Hassan.