TEUZI LEO 11.12.2021

Rais Samia Suluhu Hassan amemteua Balozi Ali Idd Siwa kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini ya Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF).


Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa leo na Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais Ikulu, Jaffar Haniu, uteuzi huo umeanza Desemba 7, 2021 ambapo Balozi Siwa ameteuliwa kwa kipindi cha pili kushika nafasi hiyo baada ya muda wa bodi hiyo kuisha Septemba 21, 2021.


Taarifa hiyo imeongeza kuwa pia Rais Samia amewapangia vituo vya kazi mabalozi wanne kwenda kuiwakilisha Tanzania katika mataifa mbalimbali.


Waliopangiwa vituo vya kazi ni pamoja na Balozi Said Shaib Mussa anayekwenda Kuwait, Balozi Fredrick Kibuta anayekwenda Urusi, Balozi Said Juma Mshana anayekwenda Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) na Balozi Alex Kalua anayekwenda nchini Israel.



Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii