• Jumanne , Agosti 26 , 2025

Shule Kufungwa Kwa Muda Kuanzia Kesho Jumanne.

Waziri wa Elimu Profesa George Magoha ametoa agizo kwamba shule zifungwe kote nchini kwa wiki moja kuanzia kesho Jumanne ili kutoa fursa kwa shughuli muhimu ya uchaguzi wa Agosti 9, 2022.

Hatua hii ya serikali inamaanisha wanafunzi na walimu wataenda mapumziko ya mapema kuliko jinsi ilivyokuwa imeratibiwa kwamba waanze likizo fupi Ijumaa wiki hii.

“Jinsi mnavyojua, Kenya itaandaa uchaguzi Jumanne, Agosti 9, 2022. Hivyo basi baada ya kufanya mashauriano, ninatangaza kwa niaba ya serikali kwamba shule zote zifungwe kuanzia Jumanne, Agosti 2  hadi Jumatano, Agosti 10 ili kuhakikisha kwamba matayarisho ya uchaguzi na hatimaye uchaguzi wenyewe unafanyika bila matatizo yoyote,” Profesa Magoha amesema.

Wanafunzi watarejea shuleni Alhamisi, Agosti 11, 2022.

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii