Biden amsalimu Kim na kusema Marekani 'imejiandaa' kwa majaribio ya silaha za Korea Kaskazini.

Rais wa Marekani Joe Biden ameondoka Korea Kusini na kuelekea Japan leo Jumapili. Biden ametoa salamu na ujumbe mfupi kwa rais wa Korea Kaskazini Kim Jong Un kuwa serikali yake ipo tayari kwa mazungumzo na Pyongyang licha ya dhamira ya kuongeza luteka zake za kijeshi na Korea kusini. Biden amesema hataki kujishughulisha na majaribio mapya ya makombora ya Korea Kaskazini wakati akiwa katika eneo hilo, jambo ambalo maafisa wa Marekani wameonya mara kwa mara kuwa wako tayari kwa lolote. Rais huyo wa Marekani ametoa ofa ya chanjo ya UVIKO-19 kwa Korea Kaskazini pamoja na China lakini amewaambia waandishi wa habari kuwa hajapata jibu lolote. Hata hivyo Korea Kaskazini imesema nia ya Marekani si ya kweli kwa sababu nchi hiyo bado inashikilia vikwazo na sera za uhasama dhidi yake.

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii