Taasisi ya habari na teknolojia ya Trump inatarajia kuzindua programu hiyo ya mitandao ya kijamii uitwayo Truth Social mapema mwaka ujao.
Haya yanajiri wakati Bw Trump akiwa amepigwa marufuku kutoka kwa Twitter na Facebook kufuatia shambulio la Ikulu ya Marekani mwezi Januari.
"$1bn imetuma ujumbe muhimu kwa makampuni makubwa yateknolojia kwamba udhibiti na ubaguzi wa kisiasa lazima ukomeshwe," alisema.
"Kadiri karatasi yetu ya usawa inavyoongezeka, taasisi ya Trump Media & Technology itakuwa katika nafasi nzuri ya kupambana dhidi ya udhalimu wa makampuni makubwa ya teknolojia."
Bw Trump alitangaza mipango ya kuzindua mtandao wa Kijamii wa Truth (Ukweli ) mapema mwaka huu, akisema itaruhusu mazungumzo "bila ubaguzi kwa misingi ya itikadi za kisiasa".
Kampuni ya habari na teknolojia ya Trump inashirikiana na Digital World Acquisition katika mradi huo.
Siku ya Jumamosi, walisema wamechangisha $1bn kutoka kwa "kundi tofauti la wawekezaji wa taasisi" bila kufichua wao ni nani.
Kwa mujibu wa ripoti, mradi huo wa mitandao ya kijamii sasa una thamani ya karibu $4bn.
Inasisitiza uwezo wa rais huyo wa zamani wa Marekani kuvutia uungwaji mkono mkubwa wa kifedha licha ya utata uliozingira wakati wake wa uongozi.