Hoja ya kumkamata Mrosso imeibuliwa na Wakili Msomi Fridolin Bwemelo ambapo amesema inafikirisha kuona aliyetoa rushwa yupo huru uraiani huku wanaoshtakiwa kwa kutoa rushwa wapo mahabusu.
Wakili Bwemelo akinukuu baadhi ya vifungu vya sheria amesema, Sheria ya kudhibiti na kupambana na rushwa kifungu 15, kifungu kidogo cha 1b imeeleza wazi kuhusu mtu anaetoa rushwa na hakuna mahali kinasema mtu amelazimishwa kutoa rushwa na kwa maana hiyo kutoa ni kutoa tu.
Amesisitiza kuwa maombi yao kama utetezi ni kuondoa utata katika jamii yenye sera ya Kazi iendelee na kuepuka upendeleo wanaiomba mahakama ichukue hatua kwa kuwa Shahidi huyo amekiri mara kadhaa chini ya kiapo kwamba ametoa rushwa kwa kulazimishwa.
“Mheshimiwa Hakimu sheria inasema kuwa Hakimu anaweza kumkamata au kutoa amri ya kukamatwa kwa mtu yoyote anayekiri kutoa rushwa na ikiwa mahakama imejiridhisha mtu huyo ametenda kosa hilo”
Ameongeza kwamba mahakama ya Hakimu Mkazi Arusha itajiridhisha vipi kwamba Mrosso ametoa rushwa ni kwa yeye mwenyewe kukiri chini ya kiapo kwamba alitoa rushwa kwa kulazimishwa, kupitia mawakili na wa serikali na wa kujitegemea kwa nyakati tofauti tofauti, shahidi alisema ametoa rushwa na hata taratibu zote zilizotumika kupeleka kesi hiyo mahakamani na kwamba iliripotiwa polisi na kupelelezwa TAKUKURU na hata kushangaa kwanini mawakili waliopo ni wa Jamhuri na sio wa TAKUKURU.
Wakijibu hoja hiyo, Wakili Tarsila Gervas kwa niaba ya Mawakili waandamizi wa Jamhuri, amesema kutokana na wao kutuhumiwa hawatakuwa na majibu isipokuwa watawasiliana na Mkurugenzi wa mashtaki (DPP) alete watu sahihi kwa ajili ya kutoa majibu ya hoja hizo.
“Mh. Hakimu tunaomba wiki mbili tuwasiliane na aliyetutuma kufanya kazi hii. Kwa sababu hata sisi ni watuhumiwa hapa. Itabidi aje mtu sahihi atakayeweza kutoa muongozo".
Hoja ya kumkamata Mrosso imeibuliwa na Wakili Msomi Fridolin Bwemelo ambapo amesema inafikirisha kuona aliyetoa rushwa yupo huru uraiani huku wanaoshtakiwa kwa kutoa rushwa wapo mahabusu.
Wakili Bwemelo akinukuu baadhi ya vifungu vya sheria amesema, Sheria ya kudhibiti na kupambana na rushwa kifungu 15, kifungu kidogo cha 1b imeeleza wazi kuhusu mtu anaetoa rushwa na hskuna mahali kinasema mtu amelazimishwa kutoa rushwa na kwa maana hiyo kutoa ni kutoa tu.
Amesisitiza kuwa maombi yao kama utetezi ni kuondoa utata katika jamii yenye sera ya Kazi iendelee na kuepuka upendeleo wanaiomba mahakama ichukue hatua kwa kuwa Shahidi huyo anekiri mara kadhaa chini ya kiapo kwamba anetoa rushwa kwa kulazimishwa.
“Mheshimiwa Hakimu sheria inasema kuwa Hakimu anaweza kumkamata au kutoa amri ya kukamatwa kwa mtu yoyote anayekiri kutoa rushwa na ikiwa mahakama imejiridhisha mtu huyo ametenda kosa hilo”
Ameongeza kwamba mahakama ya Hakimu Mkazi Arusha itajiridhisha vipi kwamba Mrosso ametoa rushwa ni kwa yeye mwenyewe kukiri chini ya kiapo kwamba aliyoa rushwa kwa kulazimishwa, kupitia mawakili na wa serikali na wa kujitegemea kwa nyakati tofauti tofauti shahidi alisema ametoa rushwa na hata taratibu zote zilizotumika kupeleka kesi hiyo mahakamani na kwamba iliripotiwa polisi na kupelelezwa TAKUKURU na hata kushangaa kwanini mawakili waliopo ni wa Jamhuri na sio wa TAKUKURU.
Wakijibu hoja hiyo, Wakili Tarsila Gervas kwa niaba ya Mawakili waandamizi wa Jamhuri, amesema kutokana na wao kutuhumiwa hawatakuwa na majibu isipokuwa watawasiliana na Mkurugenzi wa mashtaki (DPP) alete watu sahihi kwa ajili ya kutoa majibu ya hoja hizo.
“Mh. Hakimu tunaomba wiki mbili tuwasiliane na aliyetutuma kufanya kazi hii. Kwa sababu hata sisi ni watuhumiwa hapa. Itabidi aje mtu sahihi atakayeweza kutoa muongozo.
Hakimu Mwandamizi, Dkt. Patria Kisinda ameahirisha shauri hilo mpaka Disemba 2, 2021.