Waziri wa Afya, Dkt Dorothy Gwajima amesema kuwa Tanzania ni miongoni mwa nchi mbalimbali Duniani zilizojiandaa kukabiliana na tishio la wimbi la nne la ugonjwa wa Uviko-19 ambalo limegundulika nchini Afrika kusini likiwa katika anuwai mpya iliyotambulika kwa jina la OMICRON.
.
Waziri Gwajima amesema hayo baada ya kuripotiwa kwa taarifa za kuenea kwa ugonjwa huo kutoka nchi mbalimbali Duniani ambazo zimeripoti kuwa na ongezeko la visa vipya vya Uviko-19.
Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii