SIMBA WAVUNA USHINDI KWA MKAPA DHIDI YA RED ARROWS

TIMU ya Simba ya Tanzania imeibuka na ushindi wa 3-0 dhidi ya Red Arrows ya Zambia katikap Uwanja wa Benjamin Mkapa, jijini Dar es Salaam. 

Mchezo huo, umepigwa leo Jumapili, tarehe 28 Novemba 2021, kuwania kuingia hatua ya makundi Kombe la Shirikisho Afrika huku ikishuhudia Red Arrows mchezaji wake akipigwa kandi nyekundi.

Ni mchezo ambao umeshuhudia Bernard Morrison akicheza kadanda safi na lenye kuvutia kwa kufunga magoli mawili, kutoa pasi ya goli pamoja na kukosa mkwaju wa penati.

Dakika 90 zimemalizika kati ya 180 ambapo, tarehe 5 Desemba 2021, Simba watasafri kwenda Zambia kwa mchezo wa marejeo na kuhitmisha dakika zingine 90.

Richa ya mvua kunyesha na kupelekea uwanja kuwa na maji mengi, laikini bado Simba SC, iliendelea kuutawala mchezo huo.

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii