KOCHA MPYA SIMBA ATAMBA KUONDOKA NA ALAMA TATU KESHO

Kocha mpya wa Simba Pablo Franco raia wa Hispania amesema licha ya ubora wa Ruvu Shooting kwa namna alivyowaona watapambana kupata alama tatu muhimu.

“Tunategemea mchezo mgumu lakini tuko tayari kwa mchezo wa kesho. Tunajua ni mchezo muhimu na tutapambana ili tupate alama tatu.”- Kocha Pablo Franco.

Kesho NBC Premier League itaendelea kwa michezo mitatu kupigwa majira ya saa 10:00 Jioni kwa saa za Afrika mashariki.


Mbali na mchezo wa Ruvu Shooting dhidi ya Simba utakaofanyika Uwanja wa CCM KIRUMBA Mwanza, Polisi Tanzania watacheza na Coastal Union huku Tanzania Prisons wakiwakaribisha Mbeya kwanza kwenye mchezo huo wa mzunguko wa 6.


Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii