Karibia wachimba madini 72 wameripotiwa kuuawa katika mashambulio ya angani katika eneo linalozozaniwa kwenye mpaka kati ya Sudan na Misri kwa mujibu wa ripoti ya shirika la haki za bindamu nchini Sudan.
Shirika hilo ambalo linafuatilia matukio ya ukiukaji wa haki za binadamu katika vita vya Sudan, limelituhumu jeshi la Misri kwa kutekeleza shambulio hilo.
“Ndege za kijeshi za Misri ziliwalenga wachimba madini raia kaskazini mwa Mji wa Wadi nchini Sudan ambapo kwa mujibu wa taarifa za awali, watu 72 waliuawa.” Lilisema shirika hilo la haki za binadamu lenye makao yake jijini Khartoum kupitia kwa ujumbe wake kwenye mtandao wa X.
Licha ya ripoti ya shirika hilo la haki za binadamu, Msiri kwa upande wake haijazungumzia ripoti hiyo.
Shambulio hilo lilikuwa na pili mwaka huu kwenye eneo hilo ambalo shughuli nyingi za uchimbaji madini ya dhahabu hufanyika.
Shambulio kama hilo ambalo Misri ilituhumiwa kutekelezaa, lilisababisha vifo vya wafanyikazi 23 wa kuchimba dhahabu mwezi Juni.
Wakatu huo, jeshi la Misri lilisema lilitekeleza oparesheni kubwa dhidi ya uchimbaji madini haramu kwenye mipaka zake.
Misri na Sudan zimekuwa zikivutana kuhusu udhibiti wa eneo hilo lenye utajiri wa madini.