Uganda kuanza kuyauza mafuta yake nje ya nchi mwishoni mwa mwaka huu

Uganda imeipa mafuta yake jina la "Pearl Sweet" wakati huu Waziri wa nishati nchini humo Irene Batebe akitangaza kuwa wanatarajia kuanza kuyauza nje ya nchi kufikia mwishoni mwa mwaka huu.

Kwa mujibu wa Kampala, Vituo viwili vya mafuta magharibi mwa nchi hiyo vinavyojengwa na kampuni ya mafuta ya Ufaransa TotalEnergies na ile ya ile China vinakaribia kukamilika.

Baada ya kukamilika, Uganda itakuwa inazalisha mapipa laki 2 na elfu 30 ya mafuta kila siku.

Kiwanda cha kwanza ambacho kimepewa jina la Kingfisher, kinatarajiwa kukamilika kufikia mwishoni mwa mwaka huu, wakati kile cha Tilenga ujenzi wake ukiwa umekamilika kwa asilimia 74.

Sehemu kubwa ya mafuta hayo intarajiwa kusafirishwa kupitia bomba jipya la kusafirisha mafuta la (EACOP) lenye kilomita 1,443 kwenda pwani ya Tanzania.

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii