Mafuriko Nepal na Tibet: Vifo vyapindukia 900

Juhudi za uokoaji zinaendelea nchini Nepal na China baada ya mafuriko makubwa na maporomoko ya udongo yaliyotokea wiki iliyopita na yaliyosababisha vifo vya watu zaidi ya 900 huku wengine 4,800 wakiwa haijulikani waliko.

Maafa hayo, yaliyosababishwa na kuporomoka kwa sehemu ya barafu katika milima ya Himalaya, yamesababisha vifo vya watu 903 huku wengine 4,200 wakiwa haijulikani waliko na wanaendelea kutafutwa kwa kutumia helikopta, magari makubwa na mbwa wenye uzoefu katika shughuli za uokozi.

Waokoaji nchini Nepal, wakisaidiwa na wataalamu kutoka China, India na Korea Kusini, wanaendelea na juhudi za kuwatafuta mamia ya watu wanaoaminika kukwama ndani ya vichuguu vya mabwawa ya umeme katika wilaya za Rasuwa na Nuwakot, baada ya mafuriko makubwa yaliyokumba eneo la mpaka wa Nepal na Tibet wiki iliyopita.

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii