Watu 130 wakamatwa Tanzania kwa tuhuma za kuchochea uhalifu

Jeshi la Polisi Tanzania limesema limewakamata watu 130 kwa tuhuma za kuchochea vitendo vya uhalifu, ikiwa ni sehemu ya juhudi za kudhibiti upinzani, baada ya serikali kupiga marufuku mikutano yote ya kisiasa nchini humo kulingana na taarifa ya polisi, bado wanaendelea kuwafuatilia watuhumiwa wengine wanaohusishwa na tuhuma hizo.

Kabla ya marufuku hiyo ya mikutano ya kisiasa kutangazwa na Waziri wa Mambo ya Ndani mnamo Juni 26 Vijana wa Gen Z walipanga kuandamana Julai 7 kudai mageuzi ya kidemokrasia na haki kwa watu waliouawa katika vurugu za kabla na baada ya uchaguzi wa Oktoba 29 uwepo mkubwa wa vikosi vya usalama katika maeneo mengi ya nchi ulizuia maandamano hayo kufanyika.

Aidha mwezi Aprili mwaka huu tume ya uchunguzi iliyoteuliwa na serikali ya rais wa Jamuhuri ya Tanzania Dkt.Samia Suluhu Hassan ilisema takriban watu 518 waliuawa katika vurugu za uchaguzi zilizoelezwa kuchochewa na kuondolewa kwa baadhi ya wagombea wakuu wa upinzani kwenye mchakato wa uchaguzi.

Hata hivyo serikali ya Tanzania imeendelea kukanusha madai ya makundi ya kutetea haki za binadamu kwamba vyombo vya usalama vilitumia nguvu kupita kiasi wakati wa kukabiliana ghasia hizo.

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii