Mataifa ya Ulaya yakabiliwa na wimbi la joto kali

Mataifa ya Ulaya yanakabiliwa na wimbi la joto kali huku yakilazimika kuchukua hatua kadhaa ili kuepusha maafa.

Serikali ya Ufaransa imeviweka vikosi vya dharura na jeshi katika hali ya tahadhari kutokana na hatari ya kuzuka moto wa nyika huku ikipiga marufuku unywaji wa pombe hadharani.

Ufaransa, Ujerumani na Uhispania na zimetangaza kufuta baadhi ya michezo iliyotarajiwa kufanyika nje, kutokana na wimbi kali la joto linaloyakumba mataifa mengi ya Ulaya, ambako katika baadhi ya maeneo kunatarajiwa hadi nyuzi joto zaidi ya 40 Celsius.

Shirika la Afya Duniani, WHO, limesema zaidi ya watu 200,000 barani Ulaya wamefariki kutokana na athari zinazohusiana na joto kali  katika kipindi cha miaka minne iliyopita, huku vifo vingi vikielezwa kuwa vingeepukika.

10YrsJembefm  #Familiamoja #AhsantekwaTime

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii