Keir Starmer akabiliwa na shinikizo linalomtaka ajiuzulu

Waziri Mkuu wa Uingereza Keir Starmer anakabiliwa na shinikizo linaloongezeka la kumtaka ajiuzulu.

Hii ni baada ya mpinzani wake mkubwa katika Chama cha Labour Andy Burnham kurejea Bungeni baada ya kushinda uchaguzi wa wiki iliyopita katika jimbo la Makerfield Kaskazini Magharibi mwa Uingereza.

Baadhi ya vyombo vya habari vimeeleza kuwa Starmer huenda akatangaza kujiuzulu leo Jumatatu, taarifa iliyosambazwa pia na Rais wa Marekani Donald Trump aliyesema kuwa  anamtakia mema Starmer lakini akasema atajiuzulu kwa kuwa ameshindwa kukabiliana na masuala ya uhamiaji na matatizo ya nishati.

Waziri wa Biashara Peter Kyle amesema kuwa taarifa za Starmer kujiuzulu ni uvumi tu kwa kuwa kiongozi huyo kwa sasa anatafakari kuhusu hali halisi ya kisiasa akiamini kuwa uamuzi wowote atakaouchukua utakuwa kwa kuzingatia kwanza maslahi ya Uingereza.

10YrsJembefm  #Familiamoja #AhsantekwaTime

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii