Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran Abbas Araghchi amesema kitendo cha Israel kuendelea kukalia eneo la kusini mwa Lebanon ni kukiuka na kuyaweka matatani makubaliano ya amani kati yake na Marekani.
Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran Abbas Araghchi amesema makubaliano ya awali ya kukomesha vita kati yao na Marekani yanapaswa kuilazimisha Israel kujiondoa nchini Lebanon. Makubaliano hayo yanatarajiwa kusainiwa siku ya Ijumaa nchini Uswisi.
Kiongozi huyo ameongeza kwamba kitendo cha Israel kuendelea kukalia eneo la kusini mwa Lebanon ni kukiuka na kuyaweka matatani makubaliano hayo.
Ingawa Israel yenyewe si mshiriki wa makubaliano hayo lakini ni sehemu ya vita baada ya kujiunga na Marekani katika mashambulizi dhidi ya Iran mnamo Februari 28.
Hata hivyo, licha ya matamshi hayo ya kuitaka Israel kuondoka Lebanon, Israel kupitia kwa waziri wake mkuu Benjamin Netanyahu ilishaweka wazi msimamo wake kwamba itaendelea kubaki Lebanon kwa muda mrefu iwezekanavyo.
Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii