Timu ya taifa ya soka ya Morocco imefuzu kuingia hatua ya robo fainali baada ya kuifunga moja ya timu wenyeji wa Kombe la dunia 2026, Canada mabao 3 kwa 0. Timu hiyo sasa itakutana na Ufaransa katika hatua inayofuata.
Nyota wa mchezo huo Azzedine Ounahi alifunga mabao mawili, huku Soufiane Rahimi akiongeza la tatu katika muda wa nyongeza. Nayo timu ya Ufaransa imefuzu pia kuingia robo fainali baada ya kuibuka na ushindi wa goli 1-0 dhidi ya Paraguay. Bao pekee la Ufaransa lilifungwa na mchezaji Nyota, Kylian Mbappe kupitia mkwaju wa penalti katika dakika ya 70.
Ni zamu ya Morocco kulipa kisasi kwa Ufaransa?
Kwa matokeo hayo, Morocco na Ufaransa zitakutana Alhamisi katika mchezo wa kuwania kuingia nusu fainali. Mchezo huo unatarajiwa kuwa wa kusisimua, huku Morocco ikitafuta kulipiza kisasi baada ya kutolewa na Ufaransa katika nusu fainali ya Kombe la Dunia la mwaka 2022.
10YrsJembefm #Familiamoja #AhsantekwaTime