Kombe la Dunia 2026 litaanza rasmi Juni 11, 2026 ambapo wenyeji Mexico watafungua pazia dhidi ya South Africa katika mchezo wa ufunguzi utakaopigwa kwenye Mexico City jijini Mexico City.
Uwanja huo utaandika historia kwa kuwa wa kwanza duniani kuandaa michezo mitatu ya ufunguzi ya Kombe la Dunia baada ya kufanya hivyo pia mwaka 1970 na 1986.
Mashindano ya mwaka 2026 yatakuwa makubwa zaidi kuwahi kufanyika yakishirikisha timu 48 na jumla ya mechi 104 zitakazochezwa katika miji 16 ndani ya nchi tatu ambazo ni Mexico Canada na Marekani.
Wenyeji Mexico wataanza kampeni yao nyumbani kabla ya kucheza michezo mingine miwili ya hatua ya makundi katika viwanja vyao vya nyumbani ikiwemo mchezo mmoja katika Estadio Guadalajara.
Kwa mujibu wa ratiba iliyotolewa Mexico City Stadium wenye uwezo wa kubeba mashabiki zaidi ya 83,000 pia utaandaa mchezo wa Kundi K kati ya Uzbekistan dhidi ya Colombia pamoja na michezo ya hatua ya Round of 32 na Round of 16.

10YrsJembefm #Familiamoja #AhsantekwaTime