Mustakabali wa Oliver Glasner bado kitendawili

Kocha anayeondoka wa Crystal Palace Oliver Glasner amesema hana mpango wowote wa haraka kuhusu mustakabali wake wa kazi baada ya kuiongoza timu hiyo katika mechi yake ya mwisho.

Kwa utani ulioashiria hali yake ya furaha na utulivu Glasner amesema mpango wake kwa sasa ni "kuruka na kurejea London akiwa na maumivu ya mwili” baada ya kusherehekea mafanikio aliyoyapata na kikosi hicho.

Glasner aliiongoza Palace kuchukua ubingwa wa Conference League kwa ushindi dhidi ya Rayo Vallecano ikiwa ni taji la tatu la klabu hiyo tangu alipochukua usukani mwaka 2024 — ikiwemo Kombe la FA Cup na Ngao ya Jamii.

Tangu kutangaza kuondoka kwake mwezi Januari kumekuwa na uvumi kuhusu wapi Glasner anakoelekea ripoti mbalimbali zimehusisha jina lake na klabu kadhaa za ligi kuu ya Uingereza huku zingine zikidai huenda akarejea Bundesliga nchini Ujerumani.


 Hata hivyo amesisitiza kuwa hataki kufanya maamuzi ya haraka akisema kwa sasa anataka kufurahia mafanikio ya timu yake na kusherehekea na wachezaji wake.

Hata hivyo kwa kuchukua ubingwa wa Conference League Crystal Palace sasa itashiriki michuano ya ligi ya Ulaya Europa League  msimu ujao ikiungana na vilabu vingine vya Uingereza - Bournemouth na Sunderland katika michuano hiyo ya Ulaya.

10YrsJembefm  #Familiamoja #AhsantekwaTime

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii